Waamini wa dini ya kikristu ulimwenguni wameaswa
kutambua kwamba Mungu amemchagua mwanadamu kwa upendo wake, na kwa imani iliyo
kuu, na ata akiwa na dhambi nyingi kiasi
gani Mungu hatamuacha kabisa na anamtaka mwanadamu kutokukata tamaa,bali adumu
katika neno lake.
Hayo yamesemwa na Padre Vicent Bosel wa Shirika la Wamisionari
wa Damu Azizi ya Yesu wakati wa Mahubiri yake aliyo yatoa wakati wa Ibada ya Misa
Takatifu iliyofanyika kaitka Kanisa la Bikira Maria Mama wa Tumani Jema
lililoko ndani ya Kijiji cha Matumaini Kisasa
Jimbo Kuu katoliki la Dodoma.
Padre Bosel amesema
mungu anawapenda wanadamu wote wenye dhambi na wasio na dhambi na anawataka
waepuke nafasi za dhambi na wadumu katika neno la mungu ambalo linauwezo katika
maisha na lina uzima na uhai ndani yao.
Hata hivyo Padre Bosel amewataka wakristu kujenga
mazingira rafiki ya kupokea na kudumu katika neno la mungu , kutoka moyoni mwao, kwa imani ,upendo ,
kuanzia ngazi ya familia ,jumuiya
,kanisa na taifa kwa ujumla bali awe na tabia ya kutubu kila tunapoanguka dhambini ili kupata neema na Baraka za Mungu.
Amesema kuwa katika kipindi cha mfungo mtukufu wa
kwaresma hapo jumatano ijayo ambayo ni jumatano ya majivu waamini wanapaswa
kufunga na kutoa kile walichofunga kwa ajili ya wale wenye mahitaji zaidi ili
kujichotea Baraka na neema za mwenyezi mungu.
Aidha ikumbukwe kuwa kipindi cha kwaresma kitakachoanza siku ya jumatano ya majivu kinatupelekea kutafakari kwa kini hususani kwa kipindi hiki cha mwaka wa Jubilei ya Huruma ya Mungu ambao ulitangazwa na Papa Fransicko wa kwanza.
Ikumbukwe kuwa kipindi hiki cha kwaresma kiola mkristu anapaswa kufunga na kujitoa kwa kile alichokifunga kwa ajili ya kuwapatia wale wenye mahitaji zaidi na sio kufunga na kuchukua kile alichokifunga na kwenda kukifanyia sherehe au kukifanyia anasa za kidunia.
Post a Comment