Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto UMMY ALI MWALIMU amesema kuwa Ugonjwa wa Kipindupindu
ni janga na hivyo unapaswa kusimamiwa na kila Sekta ili kuudhibiti.
UMMY ameeleza hayo baada ya kumaliza
kikao cha pamoja na Timu ya Kuzuia na Kudhibiti Kipindupindu ya mkoa wa Dodoma
kuzungumzia mbinu na namna ya kuudhibiti Ugonjwa huo.
Katika Kikao hicho, Waziri UMMY
ameelezwa kuwa jumla ya Halmashauri tano kati ya saba zimeripotiwa kuwa na
Wagonjwa, Kondoa na Mpwapwa pekee zikiwa hazijapata Ugonjwa.
Waziri UMMY pia amesema wizara ya
afya itaendelea kutoa miongozo na utaalamu katika kuhakikisha wanapambana na
janga la ugonjwa wa kipindupindu huku akisisitiza suala hilo sio la wizara ya
afya peke yake na kuwataka viongozi wa halmashauri kusimamia sheria ndogondogo.
Hata hivyo amesema kuwa ugonjwa wa
kipindu pindu bado ni changamoto nchini huku idadi ya watu wakiongezeka
kufariki dunia kwa ugonjwa huo.
Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa
mkoa wa Dodoma, Dakta NASSOR MZEE amesema kuwa tangu kuzuka kwa Ugonjwa huo
mwezi Agosti mwaka jana mkoani Dodoma jumla ya watu miatano na mmoja
wameripotiwa kuugua ambapo kumi na watano kati yao wamefariki Dunia.
Post a Comment