February 22 vyombo kadha vya habari viliripoti kwa kuandika stori kuwa klabu ya Man United imefanya usajili wa kiungo mshambuliaji wa Lazio Felipe Anderson. Taarifa hiyo ambayo imeenea kwa kiasi kikubwa katika mitandao ya kijamii inaeleza kuwa Man United na Lazio wamekubaliana kila kitu kuhusu usajili wa kiungo huyo na kuwa anasubiri kujiunga na Man United mwisho wa msimu.
Felipe Anderson aliripotiwa kuwa usajili wake wa kujiunga na Man United
mwishoni wa msimu umekamilishwa kwa dau la euro milioni 60, stori
zilianza kuandikwa zaidi mchana wa February 22, lakini jioni ya February
22 Rais wa klabu ya Lazio Claudio Lotito amekanusha stori hizo na kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliofanyika kati ya Man United na LazioKiungo wa kimataifa wa Brazil Felipe Anderson ambae ndio alikuwa anatajwa kuwa atajiunga na Man United mwishoni mwa msimu, aliwahi kutamba na klabu ya Santos kabla ya kutua Lazio ya Italia mwaka 2013 na amecheza zaidi ya mechi 60 akiwa na klabu hiyo.
Post a Comment