NAIBU waziri wa maliasili na utalii Mhandisi Ramo
Makani amewataka watumishi wa wakala wa misitu nchini (TFS) kubadilika katika
utendaji wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama walivyo zoea katika awamu
za uongozi zilizo pita.
Makani aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa
akifungua warsha kwa wadau wa mazao ya misitu nchini iliyoandaliwa na Wizara ya
maliasili na Utalii mjini hapa.
Alisema serikali ya awamu ya tano imejipanga
katika kuhakikisha inaleta mabadiliko katika kila sekta hivyo kutokana na hali
hiyo anawaomba watumishi katika idara mbalimbali za misitu nchini kuacha
kufanya kazi kwa mazoea kwani hakuna atakae endelea kuwalea.
“Watu wanashindwa kutofautisha kati ya uzoefu na
mazoea hivyo basi wanajikuta wanafanyaka kama walivyozoea bila kuwaletea mabadiliko
yoyote wananchi wanao watumikia, Watumishi hao hawana nafasi katika Serikali
hii”alisema Makani.
Aidha lisema kuwa Rais Dk, John Magufuri
ameonyesha mfano katika utendaji wake wa kazi hivyo watumishi hawana budi kuiga
mfano huo na kuachana kabisa na suala la mazoea.
Akizungumzia juu ya suala la uvunaji wa zao la
misitu nchini aliwataka wadau wanaohusika na zao hilo kujipanga katika
kuhakikisha kuwa linakuwa endelevu tofauti na ilivyo hivi sasa katika baadhi ya
maeneo kuharibiwa kabisa.
“Watu wanavuna zao la misitu kwa wingi lakini
hakuna jitihada za kuifanya misitu hiyo kuwa endelevu ili zao hili liendelea
kuzalishwa kwa wingi na kuendelea kuliongezea kipato taifa letu mwisho wake
mtavuna nini ”alihoji.
Alisema kuwa kwa mwaka heka 372,000 za misitu
huwa zinaharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama vile
kilimo , ufugaji na uchomaji mikaa.
“Jumla ya heka hizo kwa mwaka zinaharibiwa kutokana
na mambo mbalimbali kama vile ajali za moto, ongezeko la matumizi ya mkaa
ambapo miti mingi inakatwa kwajili ya nishati hiyo inayotumiwa na idadi kubwa ya
watu nchini”alisema.
Alisema kuwa mahitaji ya zao la misitu kwa mwaka
ni Sentimita za ukubwa Millioni 62 ambapo hivi sasa zilizopo ni ni million 42
hivyo hali hiyo inaonyesha ambavyo kuna upungufu mkubwa.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa wakala wa
misitu nchini (Tfs) Juma Mgoo, alisema kuwa ili kuweza kukabiliana na uhaba wa
zao hilo la misitu wameweka utaratibu wa kupanda heka 8000 za miti kila mwaka.
Alisema kuwa mwaka jana walipanda heka 1200 za
miti katika maeneo mbalimbali lakini pia wamekuwa wakitoa elimu kwa wadau
mbalimbali wa sekta ya misitu nchini ili kuweza kuzikabili changamoto
mbalimbali za uharibifu wa misitu.
Post a Comment