Mchezaji bora bara Afrika mwaka huu
kulingana na CAF, Pierre-Emerick Aubameyang aliweka rekodi kwa kufunga
bao lake la 30 msimu huu alipoisaidia timu yake Borussia Dortmund
kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la Ujerumani baada ya kuichapa VfB
Stuttgart mabao 3-1.
Raia huyo wa Gabon Aubameyang pamoja na
mshambulizi mwenza Marco Reus, wameisaidia klabu yao ya Dortmund
kuzoa mabao 45 msimu huu na hawakulegeza kamba walipofunga bao moja kila
mmoja naye Henrik Mkhitaryan akaihakikishia Dortmund alama zote tatu.Kufuatia ushindi huo Aubameyang ameifungia Dortmund katika mechi zote za kuwania kombe la Ujerumani.
"Auba anajua kupima upinzani na kufunga wakati muhimu zaidi naamini kazi yake inaonekana kila siku aingiapo uwanjani''alisema mshambulizi mwenza Reus.
Dortmund walifuzu kwa nusu fainali yao ya tatu mfululizo kufuatia kichapo hicho huko Stuttgart ambayo haikuwa imeshindwa katika mashindano yote tangu mwezi desemba ikipoteza mechi yao ya kwanza.
Timu anayoifunza kocha mpya wa Manchester City,Pep Guardiola, Bayern Munich itakuwa mbioni kujiunga na Dortmund katika nne bora itakapopepetana na VfL Bochum .
Aidha Heidenheim inaialika Hertha Berlin katika mechi ile nyengine.
Post a Comment