
Viongozi
wa juu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Edward
Lowassa na wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, walijifungia mjini
hapa Dodoma kujadili mambo mawili mazito.
Kwa
mujibu wa taarifa toka ndani ya kikao hicho, viongozi hao walijadili
mustakabali mzima kuhusu kutangazwa kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa
Zanzibar Machi 20, mwaka huu pamoja na uamuzi wa wabunge wao kugomea
Kamati za Bunge.
Aidha,
viongozi hao baada ya kufikia uamuzi, jana usiku walikuwa na mkutano na
wabunge wa Ukawa kuwaeleza uamuzi waliofikia na nini wanachotakiwa
kukifanya wakiwa bungeni.
"Ni
kweli viongozi wa juu wamejadili mambo makubwa mawili, hatma ya
uchaguzi wa Zanzibar na kuhusu Kamati za Bunge zilivyoundwa, taarifa
kamili mtaipata baadae" kilieleza chanzo
Post a Comment