Umoja wa Ulaya umekaribia
kukubaliana juu ya makubaliano ya Schengen katika suala la kufungua
mipaka baina yao kusitishwa mpaka baada ya miaka miwili kutokana na
kufurika kwa wahamiaji na wakimbizi .Katika kikao cha mawaziri wa mambo
ya ndani wa nchi za ulaya huko Amsterdam kilichoibuka na mapendekezo
kuwa Ugiriki inapaswa kutengwa katika jumuiya ya schengen kama haitaweza
kufuata masharti yaliyowekwa.
Waziri wa uhamiaji wa
Ugiriki,Yiannis Mouzalas alisisitiza kuwa nchi yake inafanya kila
iwezalo ili kutatua tatizo la madeni yanayowasakama.Ugiriki imechoka
kusikia kuwa mipaka yao haitalindwa kwa sababu ya madeni.Umoja wa ulaya inasema ni takribani waamiaji zaidi ya elfu mbili wanaingia Ugiriki kila siku licha ya kwamba kuna bahari na kuna hali ya hewa ya kipupwe kikali.
Post a Comment