
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na wapambe wa aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya CCM, Stephen Wassira kwa madai kuwa waleta maombi hawakuwa na haki kisheria ya kufungua kesi hiyo
Wapambe wa Wassira walifungua kesi Mahakama kuu kupinga matokeo ya uchaguzi huo wakidai kuwa uligubikwa na udanganyifu na hujuma dhidi ya mgombea wao ( Stephen Wassira ) ikiwa ni pamoja na kutofautiana kwa idadi ya wapiga kura kwenye kituo na jumla ya kura zilizoonekana kwenye fomu za matokeo. Wapambe hao waliiomba mahakama kubatilisha ushindi wa Bulaya.
Bulaya alihamia Chadema akitokea CCM na kupewa nafasi ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita na hatimaye kumshinda Stephen Wassira aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mingi na waziri wa serikali ya awamu ya nne.
==>Kupitia Facebook, Esther Bulaya ameandika kuhusu hukumu ya kesi hiyo:
"Nilimshinda
Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na
wapambe wa wasira.
"Mungu
husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye
mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza
kusikiliza Hukumu.
"Mbunge wenu nipo dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho."
Post a Comment