Watu watatu wamepelekwa hospitali
kaskazini mwa Siera leone wakiwa na majeraha yaliyotokana na kupigwa
risasi baada ya kulumbana na askari juu ya mambo gani wanapaswa
kuzingatia ili kuepukana na Ebola.
Polisi wamesema walirusha
mabomu ya machozi baada ya vijana hao kuvamia kituo chao huko mjini
Barmoi,eneo ambalo mtu mmoja alikufa kutokana na Ebola wiki iliyopita.la
Nchi ya Siera leone ilitangaza kuwa iko huru na ugonjwa huo kabla ya
kifo hicho kutokea.Vijana walikuwa na hasira juu ya kufungwa kwa soko katika mji mmoja nchini humo lakini utawala ulitanabahisha kwamba ulisimamisha shughuli hizo za kibiashara kuendelea sokoni ili waweze kubaini watu watatu walipotea huku wakiwa wameathirika na ugonjwa huo.
Post a Comment