Chama cha
waendesha bodaboda Jijini Arusha ( UWAPA) chaiomba serikali kutatatua
utata uliopo kati ya waendesha bodaboda na waendesha pikipiki za kawaida
kwa kuwawekea alama maalumu ambayo itawatambulisha, hii ni kutokana na
maandamano ambayo yamefanyika siku ya tar 25./1 /2016 kwani ni kinyume
kwakuwa chama hakina taarifa yeyote kuhusu maandamano hayo.
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa UWAPA bwana Godlight Rugemalila ambapo
amesema ametoa taarifa polisi kutokana na maandamano hayo na amesema
jambo walilolifanya siyo sahihi kwa hao walioratibu maandamano hayo ,na
amewataka waendesha bodaboda wote kama kuna jambo lolote watalipata
ofisini wafuate utaratibu wasikurupuke
Amesema
kuwa yapo makundi ya aina mbili kwa waendesha bodaboda,kundi la kwanza
ni walimesajiliwa na UWAPA hawana vituo maalum , kundi la pili ni
waendesha pikipiki za kawaida hawa hawajasajiliwa na idadi yao ni kubwa
ambao huwaharibia wale ambao wanafanya biashara halali ya kubeba abiria
Amesema
kuwa wao kama UWAPA hawajapanga maandamano walipata taarifa kutoka kwa
watu binafsi na walishtushwa kusikia kuna maandamano hayo na ameongeza
kuwa wanaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili
kufahamu ni wakina nani wanahusika kuratibu maandamano hayo .
Amewataka
waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani kama
zinavyoelekeza, wawe na leseni, wavae kofia ngumu ,wapaki kwenye vituo
vilivyosajiliwa ,amewashauri abiria wanaotumia usafiri huo wachukue
bodaboda zilizopo kwenye vituo kwani akipata tatizo lolote ni rahisi
yeye kusaidika tofauti na akichukua pikipiki ambayo ameiona barabarani
inapita utakosa pa kupeleke malalamiko yako maana kila kituo kina
kiongozi.
Ameainisha
waendesha bodaboda waliosajiliwa na wanaotambulika hadi sasa jumla yao
ni 2950 ,vituo vilivyosajiliwa 144 na vituo bubu ambavyo bado na
vinatazamia kupata usajili ni 55 hivyo amewataka waendesha pikipiki wote
wajisajili kwenye chama hii ni kwa faida yao maana watatambulika
watasaidika mara wapatapo tatizo na hii itawaepusha kuingia kwenye
lawama za mara kwa mara kuwa waendesha pikipiki ni wakwapuaji na
wanatumika kwenye matukio ya uhalifu.
Amehitimisha
kwa kusema kuwa UWAPA ni umoja wa wawaendesha bodaboda jijini Arusha na
umoja huu ulisajiliwa marchi 2012 na unatambulika kiserikali,lengo ni
kuwaleta pamoja waendesha bodaboda na huwa wanapatiwa mafunzo na RTO
chini ya kitengo cha usalama barabarani , hivyo amewataka wananchi
wafahamu kuwa wapo waendesha bodaboda hawa wanapaki maeneo
yaliyoidhinishwa na ni vituo halali na waendesha pikipiki ni yeyeote
yule unayeweza mchukua barabarani hana kituo.Maandamano hayo yalifanyika kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha wakiwa na madai ya wakimtaka mkuu huyo wa mkoa atoe tamko kuhusu kusumbuliwa kwao na askari wa usalama barabarani
Post a Comment