Viongozi wa majimbo nchini Australia wametia saini stakabadhi ya kuunga mkono juhudi za taifa hilo kuwa jamhuri.
Kiongozi
pekee ambaye bado hajatia saini stakabadhi hiyo ni kiongozi wa jimbo la
Magharibi, Colin Barnett, ambaye anasema ingawa anaunga mkono juhudi za
taifa hilo kuwa jamhuri, huu sio wakati mwafaka.Raia wa Australia walipinga pendekezo la kuifanya nchi hiyo kuwa jamhuri kwenye kura ya maamuzi 1999.
Waziri mkuu wa sasa Malcolm Turnbull alikuwa kiongozi wa vuguvugu lililopigania juhudi za kutaka kuwa na jamhuri wakati huo.
Lakini tangu aingie mamlakani, Bw Turnbull amesema hakufai kuwa na mabadiliko yoyote hadi baada utawala wa Malkia Elizabeth II kumalizika.
Juhudi za sasa zinaongozwa na Peter FitzSimons ambaye amesema viongozi wote, wakiwemo Bw Turnbull na kiongozi wa upinzani Bill Shorten, wanaunga mkono kukatizwa kwa uhusiano wa Australia na utawala wa kifalme wa Uingereza.
Australia kwa sasa, badala ya kuwa na rais au kiongozi wa nchi, humtambua kiongozi wa kifalme wa Uingereza kama kiongozi wa taifa. Malkia au mfalme huwakilishwa na gavana mkuu.
Serikali huongozwa na waziri mkuu.
Post a Comment