
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, amewataka baadhi ya wabunge wa
upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze kupata
ushirikiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January
Makamba amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama cha Mapinduzi ndiyo
wenye dola na wao ndiyo wanaongoza serikali hivyo amewataka baadhi ya
wabunge wa upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze
kupata ushirikiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali hiyo pindi
watakapo hitaji msaada wowote kutoka serikalini.
January
Makamba amesema hayo bungeni na kudai amefadhaishwa na michango ya
wabunge wa upinzani ambao walikuwa wakitumia lugha za kuudhi dhidi ya
Rais pamoja na viongozi wa serikali.
"Najua
kazi ya upinzani ni kulaumu hivi nyinyi wapinzani kwa kazi anayofanya
Rais Magufuli leo mngepewa nafasi wapinzani ni kipi ambacho mngefanya
zaidi ya hiki? "Alihoji January Makamba
Lakini
katika hatua nyingine amesema aina ya uchangiaji nyingine ya wabunge
bungeni ni kama walikuwa wakiwatisha watanzania juu ya sakata la
Zanzibar na alimaliza kwa kusema kuwa utatuzi wa suala la Zanzibar
haupatikani barabarani, haupatikani bungeni bali unapatikana katika
Katiba na sheria za Zanzibar pekee na si kitu kingine.
Post a Comment