Taasisi
ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), imewafikisha mahakamani
watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akiwamo Mkurugenzi
mtendaji, Upendo Sanga kwa madai ya kuhujumu uchumi.
Awali, Sanga alifika mahakamani hapo kusikiliza hukumu ya kesi yake iliyofunguliwa na Takukuru mwaka 2014.
Baada
ya hakimu kumwaachia huru, Takukuru walimzunguka na kumkamata tena na
maofisa wake ambao walipandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwendesha
Mashtaka wa Takukuru, Sarah Martin aliwasomea mashtaka washtakiwa hao,
Mweka Hazina, Hafidhi Mgagi, Mhasibu Gershom Bwire na Sanga.
Sarah
alidai kuwa washtakiwa hao walimdanganya mwajiri wao na kujipatia fedha
kwa kutumia nyaraka za kughushi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh4
milioni.
Mwendesha
mashitaka huyo alidai kuwa Sanga na Mgagi kati ya Novemba 23 hadi 28,
2012 waliidhinisha malipo ya Sh4 milioni kwa Gershom Bwire kutengeneza
vitabu 150 vya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
Alidai
kuwa katika shtaka la pili mshtakiwa wa tatu, Bwire Novemba 23 na 28,
2012 alijipatia fedha isivyo halali, mali ya mwajiri.
Mwendesha mashtaka alidai kuwa washtakiwa hao wameitia hasara halmashauri kwa kujipatia Sh4 milioni.
Post a Comment