Misioni ya Umoja wa mataifa iliyoko
mji wa Darfur nchini Sudan inasema watu zaidi ya elfu kumi wamekimbia
makazi yao kutokana na mapigano baina ya majeshi ya serikali na waasi.
Misheni
hiyo ya umoja wa mataifa inasema inajaribu kupata uhakika zaidi wa
taarifa kuhusu watu wengine waliotekwa katika mapigano yaliyokuwa
yakiendelea katika milima ya Jebel Marra katikati ya mji wa
Darfur.Walinzi wa amani wa umoja wa mataifa wametaarifu kuwa pamekuwa na
milipuko mikubwa ya moto na mabomu katika eneo hilo siku ya jumamosi.Umoja wa mataifa unakadilia kuwa kuna watu zaidi ya milioni mbili ambao wamekimbia makazi yao mjini Darfur kutokana na hali ya eneo kutoweza kuimarika tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ilipoanza mwaka 2003.
Post a Comment